Magonjwa yanayoweza kupatikana kwenye maji

Tafsiri

Magonjwa ya kwenye maji ni magonjwa yanayopatikana ama kusambazwa kupitia maji. Magonjwa haya ni kama vile homa ya matumbo, kipindupindu, kuhara na kuhara damu. Kama maji si safi na salama kwakuwa yamechanganyikana na maji taka basi kuna uwezekano mkubwa wa mtumiaji kupata maambukizi.

Kinga

Inashauriwa kuchemsha maji au kuyavukiza kabla ya kuyatumia ili kuhakikisha maji ni safi na salama. Pia maji huweza kufanywa safi na salama kwa kutumia dawa kama waterguard.

Ukurasa huu ni kipisi tafadhali saidia kuendeleza!

This article is issued from Appropedia. The text is licensed under Creative Commons - Attribution - Sharealike. Additional terms may apply for the media files.